Nafasi Ya Matangazo

April 14, 2014

WATU 15 wamenusurika kufa mara baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa bomu lililotengenezwa kwa mkono kulipuka katika  bar ya Arusha Night Park
iliyopo maeneo ya mianzini mjini hapa.

Tukio hilo lilitokea april 13  majira 1;30 jioni   mara baada ya watu hao kupumzika katika baa hiyo kwa lengo la mapumziko ya wikiendi huku wengine wakiangalia mpira.

Akizungumza mara baada ya kutembelea majeruhi hao katika hosipitali ya Selian mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa tukio hilo limetokea bila kuwepo kwa mitazamio yeyote.

Mulongo alieleza kuwa katika tukio hilo watu walikuwa wanaendelea na kazi zao na ndipo mara waliposikia kitu kama kishindo na ghafla ndipo watu hao walipoanza kurupushani za hapa na pale kutokana na tukio hilo.

Alisema kuwa, mara baada ya  tukio hilo polisi walifika eneo la tukio na kuwachukua majeruhi hao na kuwapelekea katika hospitali ya Mount Meru, Selian, na hospitali ya st.elizabeth kwa ajili ya kupata matibabu.

Aidha katika majeruhi hao watatu wamesharuhusiwa na wengine  12 wanaendelea na matibabu huku mmoja kati yao akiwa na majeraha makubwa
kwenye miguu ambaye alikuwa karibu na eneo bomu lililopotegeshewa .

Aidha Mkuu wa mkoa wa Arusha alitoa rai kwa watanzania kutoa ushirikiano kwa jeshi pale wanapokuwa na taarifa za mtu yeyote kuhusika na tukio hilo.

Mulongo alisema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea kupitia kamera zilizofungwa kwenye bar hiyo katika kuwatambua wale wote waliohusika na tukio .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti majeruhi waliolazwa katika  hospitali ya Mount Meru ,ambaye  ni mhudumu Luis John alisema kuwa, alishtukia kishindo na moshi mkubwa wakati akihudumia wateja  na watu kukimbia bila mwelekeo.

Aidha alisema kuwa , bomu hilo lilirushwa ndani ya bar hiyo ambapo asilimia kubwa ya wateja walikuwa wakiangalia mpira na ndio wengi wao waliojeruhiwa kutokana na bomu hilo. Aidha  baadhi ya majeruhi hao waliojeruhiwa ambao ni wahudumu wa bar hiyo ni Suzan John, Joyce William, na Meneja wa bar hiyo aliyetambulika kwa jina la Halima .

Hata hivyo hivyo baadhi wa wananchi wakizungumzia tukio hilo walisema kuwa matukio ya kulipuka kwa mabomu mkoani Arusha yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kusababisha kuwepo kwa hofu kubwa miongoni mwa wananchi.

Mwananachi huyo aliyejitambulisha kwa jina la ,Ashura Salimu mkazi Soweto alisema kuwa, matukio hayo yamekuwa yakiwafanya kuishi kwa wasiwasi mkubwa ,kwani yamekuwa yakijirudia mara kwa mara.

Hivyo aliomba serikali kuhakikisha kuwa inakuwa makini na kuchukua hatua za haraka kwa watu hao ambao wamekuwa wakihusika na matukio hayo kwani kwa mkoa wa Arusha imekuwa ikizua wasiwasi mkubwa .

Aidha itakumbukwa kuwa hili ni bomu la nne kurushwa kwenye mikusanyiko
ya watu ambapo bomu la kwanza lilirushwa kanisa la katoliki la Joseph Mfanyakazi liilopo  olasiti katika uzinduzi wa kanisa hilo,huku tukio la pili lilirushwa katika viwanja vya Soweto katika mkutano wa kufunga kampeni za chadema , na la tatu likirushwa katika mkesha wa mwaka mpya katika kanisa katoliki usa river .
Posted by MROKI On Monday, April 14, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo