Nafasi Ya Matangazo

August 17, 2013



Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza udhamini wa Castle Lager kwa klabu ya FC Barcelona  ya nchini Hispania, (kushoto) ni  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kushilla Thomas.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kushilla Thomas (kushoto), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza udhamini wa Castle Lager kwa klabu ya FC Barcelona  ya nchini Hispania, kulia ni Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo. 

                                                                                               *******
Baada ya kutangazwa kwa udhamini wa miaka mitatu wa bia ya Castle Lager kwa moja ya FC Barcelona, moja ya klabu maarufu zaidi duniani, leo hii udhamini huo unazinduliwa rasmi hapa Tanzania.  huu unafanyika.

Udhamini huu unaifanya Castle Lager kuwa Bia rasmi ya FC Barcelona barani Afrika hususani hapa Tanzania na nchi nyingine 10 barani Afrika ambapo Castle Lager itakuwa kinywaji rasmi pia kwenye shughuli zote za klabu ya FC Barcelona katika nchi hizi. 

“Udhamini utaleta manufaa mengi kwa wanywaji wa Castle Lager na mashabiki wa FC Barcelona nchini Tanzania kupitia promosheni mbalimbali na hii itaongeza umaarufu wa timu hii hapa Tanzania na barani Afrika kwa ujumla,” alisema Kushilla Thomas, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania. 

Hii ni mara ya kwanza kwa FC Barcelona kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya Kiafrika jambo ambalo litawafungulia milango mashabiki wa FC Barcelona nchini Tanzania na nchi nyingine barani kuweza kupata bidhaa, matukio ya kukumbukwa na nafasi za kushinda safari safari ya kwenda Barcelona Hispania kuitembelea klabu. 

“Tumefurahi kusaini mkataba na Castle Lager, chapa inayofahamika dunia nzima. Tunafanana mila na desturi na Castle Lager na sote tuna historia ya miaka zaidi ya 100. Pia kama tulivyo sisi Barcelona, bia ya Castle Lager ina mapenzi makubwa kwaa mpira wa miguu pamoja na mashabiki barani Afrika,” alisema Javier Faus, Makamu wa Rais wa Barcelona anayeshughulikia Uchumi.

Castle Lager imekuwa ikijihusisha na na mpira wa miguu barani Afrika kwa muda wa miaka 85 ambapo hivi sasa inadhamini ligi za soka katika nchi za Zimbabwe, Swaziland na Lesotho. Pia Castle Lager ni mdhamini wa mashindano ya COSAFA yanayofanyika Kusini mwa Afrika na CECAFA yanayofanyika Afrika Mashariki. 

Kutokana na mpira wa Ulaya kupata umaarufu mkubwa na mashabiki barani Afrika, Castle Lager kwa miaka mingi imekuwa mdhamini wa matangazo ya mashindano mbalimbali ya mpira na kuwapatia mashabiki nafasi ya kuangalia mechi za Klabu bingwa Ulaya, ligi kuu ya Uingerereza na ligi kuu ya Hispania kupitia luninga.

Watumiaji wa CASTLE Lager pamoja na mashabiki wa FC Barcelona hapa Tanzania sasa watarajie mambo makubwa kwani udhamini huu utawaletea mambo mengi ya kusisimua. 


MASWALI NA MAJIBU KWA MKURUGENZI WA MASOKO WA TBL, BI. KUSHILLA THOMAS

1. Je Ushirikiano huu unahusu nini?
Ushirikiano huu unaifanya, Castle Lager kuwa Bia rasmi Ya Afrika inayodhamini FC Barcelona. Castle ni bia  bingwa ya Afrika ambayo inajitahidi kusimamia na kuendeleza ukamilifu/ubora wake wakati FC Barcelona ni timu bingwa ambayo daima inalenga kufikia mafanikio zaidi. Huu ni ushirikiano imara na ni matokeo ya mapenzi yetu kwenye soka

2. Unajisikiaje kuhusiana na ushirikiano huu?
Nina msisimko mkubwa kuhusiana na ushirikiano huu na FC Barcelona  na Nina furaha kusema kwamba ushirikiano huu utaimarisha uhusiano kati ya Castle Lager na wateja wake wa Afrika ambao ni mashabiki wazuri wa timu hii ambayo inaangaliwa na kufuatiliwa na wapenzi wa soka duniani kote.

3. Castle itafaidika vipi na ushirikiano huu?
Kupitia ushirikiano huu, Castle Lager itakuwa ni bia pekee Afrika yenye haki za kipekee kutumia  Nembo ya FC Barcelona, rangi, na picha za wachezaji katika mawasiliano ya bidhaa ya Castle kama vile matangazo ya aina zote nk. Tunaamini kwamba ushirikiano huu Utajenga uhusiano kati ya FC Barcelona na watumiaji wa bia ya Castle Lager.  Aidha kutakuwa na shughuli mbalimbali zinazohusu kuendeleza mpira Tanzania zikiendelea  na maeneo mengine ya Afrika inakopatikana bia ya Castle.

Bia ya Castle inatambuliwa kama mdhamini Mkuu wa mpira wa miguu na matukio mengine mengi ya michezo Afrika na kimataifa. Ushirikiano huu kati ya  Barca / Castle ni kilele cha mafanikio ya udhamini wa michezo.

4. Ina maana gani kwa mashabiki wa soka na watumiaji/wateja wa CASTLE katika
Nchi yako?

Tunataka kuhakikisha kwamba tunaimarisha undugu huu katika soka la Tanzania na hasa mashabiki wa FC Barcelona ambao ni sehemu ya ushirikiano huu wa kusisimua. Maelezo zaidi yatafafanuliwa wakati wa uzinduzi wa kitaifa jijini Dar es Salaam tarehe 17 Agosti na wapenzi wa soka wa Tanzania watashiriki katika mfululizo wa shughuli za soka za kikanda / kanda ambazo ni za kuhamasisha. Kutakuwa na shughuli za kijamii, kuwazawadia mashabiki wetu waaminifu wa Castle/Barca.  Kupitia ushirikiano huu Castle Lager itahakikisha kila shabiki anafurahia wakati kamili

5. Je Ushirikiano huo utakuwa na manufaa chanya kwenye jamii Nchini  kwako?.

Hakika, Mashabiki wa Barcelona Tanzania na jamii zao kuna mengi ya kusuburia, Castle Lager ina mipango mikubwa ya kuifikia jamii kwa maendeleo kwenye mikoa zaidi ya nane nchini. 

Tunataka kuhakikisha kwamba tunaimarisha undugu huu katika soka la Tanzania na hasa      mashabiki wa FC Barcelona ambao ni sehemu ya ushirikiano huu wa kusisimua. Maelezo  zaidi yatafafanuliwa wakati wa uzinduzi wa kitaifa jijini Dar es Salaam tarehe 17 Agosti na wapenzi wa soka wa Tanzania watashiriki katika mfululizo wa shughuli za soka za kikanda /  kanda ambazo ni za kuhamasisha. Kutakuwa na shughuli za kijamii kuwazawadia mashabiki wetu waaminifu wa Castle/Barca.  Kupitia ushirikiano huu Castle Lager itahakikisha kila shabiki anafurahia.

Posted by MROKI On Saturday, August 17, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo