Nafasi Ya Matangazo

June 16, 2013

Na Mwandishi Wetu, Arusha
KUTOKANA na mlipuko wa kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu, uchaguzi wa Kata nne jijini Arusha uliopangwa kufanyika leo umeahirishwa na kupangwa tena kufanyika Juni 30 mwaka huu.

Uchaguzi huo umeahirishwa huku mlipuko wa jana ambao ulitokea wakati Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maeendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anafunga mkutano wake, ulisababisha kuzuka kwa taharuki kubwa katika mkutano huo wa kampeni.

Watu kadhaa wamehofiwa kufa katika mlipuko huo, ambao umezidi kuomnyesha kuwa hali ya amani kataika Taifa hili la Tanzania inazidi kutoweka.

Mwandishi wetu jijini Arusha, aliiambia Handeni Kwetu kuwa uchaguzi huo umeahirishwa. Bado tunafuatilia kwa kina mtifuano huo sambamba na hali za majeruhi na waliopoteza maisha.

Mlipuko huo ulitokea na kuleta wasiwasi mkubwa katika kazi za kijamii, kama vile mikutano na makongamano pale yanapohusisha watu wengi na kuleta hofu kubwa.
Posted by MROKI On Sunday, June 16, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo