Nafasi Ya Matangazo

January 21, 2013



 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas akiongea na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani na Waandishi wa habari nje ya jengo la makao makuu ya jeshi la Polisi Mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas akiongea na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Camirius Wambura aliyeshika madawa ya kulevya aina ya mirungi nje ya jengo la Makao Makuu ya jeshi hilo mkoani hapa mara baada ya kukamata shehena hiyo.
 Gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T. 284 AGL ambalo lilikuwa na shehena aina ya mirungi viroba vipatavyo 173 vyenye jumla ya uzito wa kilogramu 1800.
 *****
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Wiki moja tu baada ya jeshi la Polisi Mkoani Arusha kukamata lori aina ya Mitsubishi Canter lililokuwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi, leo tena Jeshi hilo limekamata shehena nyingine ya madawa ya aina hiyo ambayo ilikuwa kwenye lori aina ya Fuso lenye namna za usajili T. 284 AGL

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Liberatus Sabas alisema kwamba tukio hilo limetokea leo muda wa saa 12:30 asubuhi eneo la Engarenaibo lililopo wilayani Longido ambapo madawa hayo yalikuwa yanasafirishwa kutoka nchi jirani ya Kenya kuja hapa nchini kupitia mpaka wa Namanga.

Aliongeza kwa kusema kwamba mirungi iliyokamatwa ni jumla ya viroba 173 vyenye uzito wa kilogramu 1800 na mafanikio hayo yalipatikana baada ya jeshi hilo kupata taarifa toka kwa raia wema na mtu mmoja alikamatwa na anaendelea kuhojiwa huku mwingine akifanikiwa kukimbia.

Baadhi ya viroba hivyo vilionekana kuwa na majina ya watu, uzito na mahali, hali inayotafsiriwa kuwa huwa vinagawanywa kwa watu hao mara baada ya kuingizwa mjini hapa.
Kamanda Sabas aliendelea kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kwa ushirikiano wao mkubwa na kuwaomba waendelee kushirikiana na jeshi hilo hali ambayo itasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu.
Pia Kamanda Sabas aliwaonya wamiliki wa vyombo vya usafiri hasa magari kutokubali vyombo vyao vitumike katika usafirishaji wa biashara haramu kwani pindi vinapokamatwa huwa vinakuwa chini ya vyombo vya dola huku kesi ikiendelea badala ya kuendelea kufanya kazi nyingine za uzalishaji. Mpaka hivi sasa kwa muda wa wiki moja ndani ya mwezi huu jumla ya magari mawili yamekamatwa.
Posted by MROKI On Monday, January 21, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo