Nafasi Ya Matangazo

December 24, 2012

MAGAZETI mengi ya leo katika ukurasa wake wa mbele licha ya kuwa na habari zaidi ya moja iliyopewa uzito wa kuuzia gazeti husika lakini pia kuna habari iliyopewa kichwa ‘OFISA WA TAKUKURU AMUUA MWENZAKE KWA RISASI’.

Habari hiyo inamhusu Ofisa  wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bhoke Ryoba, aliyefariki dunia  baada ya kupigwa risasi na ofisa mwenzake wakati wakisherekea ufukweni mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.

Father Kidevu Blog , baada ya kupitia habari hizo katika magazeti kadhaa lakini ilikutana na mkanganyiko juu ya habari hizo hasa kufuatia kuwapo kwa kauli mbili tofauti juu ya aliyehusika kumuua Ryoba.

 Ingawaje magazeti Mengi yamemnukuu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke. Engelbet Kiondo, na kusema bayana kuwa  Ryoba alipigwa risasi na ofisa mwenzake, Mussa John (34), mkazi wa Mabibo, jijini Dar es Salaam.

Pia baadhi ya magazeti yalinukuu taarifa ya Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dkt. Edward Hoseah, iliyosema wazi kuwa Ryoba alifariki juzi jijini Dar es Salaam baada ya kupigwa risaasi.

Sehemu ya nukuu katika gazeti la Nipashe ilisema hivi, “Tumekuwa tukipokea simu nyingi kutoka kwa watu wakihitaji kufahamu ukweli wa tukio la kupigwa risasi kwa mtumishi Bhoke Ryoba, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, anapenda kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hili kwamba ni kweli alifariki dunia Jumamosi (juzi) usiku baada ya kupigwa risasi,” ilieleza kwa kifupi taarifa hiyo.

Hata hivyo, taarifa ya Takukuru haikueleza chanzo cha mtumishi huyo kupigwa risasi wala eneo lilipotokea tukio hilo, lakini iliongeza kuwa uchunguzi kuhusu chanzo cha tukio hilo bado unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi.

Father Kidevu Blog, imekumbwa na wasiwasi juu ya utoaji wa taarifa hizi hasa kutoka Ofisi Husika ambayo Marehemu alikuwa akifanyia kazi. Hofu hii ni kwanini TAKUKURU itoe taarifa zinaoelea zisiszo za kiuchunguzi kama ofisi yao ilivyo ama kwakuwa wao hawachunguzi mauaji?

Lakini kama hilo haliwahusi Dkt. Hoseah alikuwa pia anauwezo mkubwa sana wa kuwasiliana na Jeshi la Polisi likampa taarifa za awali juu ya mauaji hayo yalivyo tokea ili aitumie taarifa hiyo kutoa ufafanuzi kwa Umma kupitia vyombo vya habari.

Gazeti la Mwananchi mbali na kuandika habari hiyo kwa kutumia Taarifa ya Mkurugenzi wa TAKUKURU, lakini pia waliongea na Ofisa habari wa Takukuru Doreen Kapwani na kutoa ufafanuzi zaidi juu ya tukio hilo na kuzidi kujiweka wazi kwa tasisi hiyo nyeti kuwa haikuwasiliana na Polisi ama walikuwa wanataka kuepusha kikombe hicho cha kuipa jamii taarifa sahihi na za ukweli.

Kapwani, aliwafafanulia Gzeti la Mwananchi kuwa ofisa huyo mchunguzi alifikwa na umauti wakati anajumuika na marafiki zake katika moja ya tafrija iliyokuwa ikifanyika katika eneo la Kigamboni.

Alisema akiwa katika hafla hiyo, ghalfa walitokea watu wasiojulikana na kumiminia risasi hadi kufa.

Gazeti la Mwananchi lilimemnukuu Kapwani “Hawa watu walimvamia Ryoba aliyekuwa kwenye sherehe moja na kumshambulia kwa risasi na kisha wakatokomea kusikojulikana,” alisema na kuongeza:

“Watu hao hawakutambulika kwa kuwa baada ya kutekeleza azma hiyo walitoweka haraka na kutokomea.”

Polisi wao kupitia Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke. Engelbet Kiondo ilisema kuwa tukio hilo lilitokea katika eneo la ufukwe wa Hoteli ya Southern Beach saa 1:30 usiku wakati watumishi wa Takukuru walipokwenda kuburudika.

Kwa mujibu wa Kamanda Kiondo, wakati watumishi hao wakiburudika, ndipo mmoja wao, Mussa John, alipochukua bastola yake na kuanza kupiga risasi hewani.

Alifafanua moja kati ya risasi hizo, ilimpiga Ryoba na kumsababishia majeraha kifuani.

Baada ya kujeruhiwa, Ryoba alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu, lakini alifariki dunia usiku wa kuamkia jana wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo, John alikwenda kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Chang’ombe na anaendelea kushikiliwa.

Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Ahmed Msangi, na maafisa wengine wa polisi walikwenda eneo la tukio.

Kamanda Kiondo alisema katika mahojiano na polisi, John alisema kuwa alimpiga risasi marehemu kwa bahati mbaya.

Kamanda huyo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Father Kidevu Blog ilidhani kuwa vyombo hivi viwili hasa TAKUKURU ingefanya mawasiliano kwanza na Polisi ili kupata taarifa kamili ya tukuo hilo namna ilivyotokea hadi kufa kwa mtumishi wake kabla ya kutoa taarifa zinaolea.

Ona sasa TAKUKURU wanauambia Umma kupitia vyombo vya Habari kuwa Ryoba kauwawa na watu wasio julikana ilhali Polisi wanasema wazi anaedaiwa kumuua Rhoba ni John na amejisalimisha mwenyewe katika kituo kimoja wapo cha Polisi jijini Dar es Salaam kwa usalama zaidi.
Posted by MROKI On Monday, December 24, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo