Nafasi Ya Matangazo

December 24, 2012

Na Mwandishi Wetu
Msondo Ngoma na Mlimani Park Orchestra “Sikinde” leo mchana zitachuana vikali katika ukumbi wa Equator Grill, Temeke.

Mpambano huo wa kusherekea sikukuu ya Krismasi litakuwa la kufunga mwaka 2012 na pia litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wa muziki wa dansi nchini mwaka huu.

Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litanzaza saa tisa alasiri hadi majogoo.

Bendi hizo zitapiga katika jukuwaa moja lakini kila moja itatumia vyombo vyake vipya walivyopewa na Konyagi hivi karibuni ili kuondoa malalamiko ya hujuma.
Kapinga alisema kila bendi itapiga kwa muda wa saa moja kabla ya kuipisha bendi nyingine.

Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera alisema jana kuwa watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaibuka kidedea.

Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni 'Nimuokoe Nani', 'Zarina', 'Mwanaidi', 'Kanjelenjele', 'Bahati', 'Sesilia', 'Usiue Usiibe', 'Asha Mwana Seif', 'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli Moto', 'Kilio cha Mzima', 'Ajali' na 'Suluhu'.

Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede, Mabera, Abdul Ridhiwani Pangamawe, Saad Ally 'Mashine', Eddo Sanga, Huruka Uvuruge, Zahoro Bangwe, Ibrahim Kandaya, Ismail Mapanga, James Mawilla, Muhidini Gurumo, Eddo Sanga, Juma Katundu, Hamisi Mnyupe, Roma Mng’ande `Romario’ na Hassan Moshi.

Naye kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.

“Tuna waimbaji wazuri na vyombo vipya na hakuna kitakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.

Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni 'Selina', Wiki endi', 'Penzi la Fukara', 'Hiba', 'MV Mapenzi’, 'Supu Umelitia Nazi' na 'Jinamizi la Talaka'.

Sikinde inaundwa na wanamuziki kama Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Kaingilila Maufi, Tonny Karama, Shaaban Mabuyu, Habib Abassi, Juma Choka, Ally Jamwaka, Athumani Kambi, Mbaraka Othman, Hamisi Milambo, Shaaban Lendi, Joseph Benard, Ramadhani Mapesa na Habibu Jeff.

Pambano umeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi.
Posted by MROKI On Monday, December 24, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo