Nafasi Ya Matangazo

November 06, 2012




Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba cha Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.

Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akipandishwa kwenye Gari ya Wagonjwa kwa lengo la kuwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dare es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

*********

Na Ali Issa na Mwanaisha Mohamed  
Maelezo Zanzibar 

Naibu Mufti Mkuu wa  Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi amesema kitendo cha kumwagiwa Tindikali Katibu wa Mufti Mkuu Sheikh Fadhili Soraga si kitendo cha kiungwana na hakiendani kabisa  na utamaduni na mila ya  dini ya kiislamu .

Hayo ameyasema leo huko Ofisini kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar  wakati alipokutana na waandishi wa habari kufuatia  tukio la kujerihiwa vibaya  katibu huyo kwa kumwagiwa tindikali  na watu wasio julikana katika maeneo ya Kwerekwe kwenye kiwanja cha mpira  alipokuwa akirudi mazoezi alfajiri ya leo.   

 Amesema kitendo hicho sio cha kiungwana na hakiendani na maadili ya uislamu kwani dini ya kiislamu siku zote ina amrisha kutenda mema na kukatazana Mabaya .  “Uislamu ni Dini ya amani, upendo na kuaminiana na hawi mmoja wenu muumini wa kweli mpaka ampendelee mwezake mema”alisema Naibu Mufti .

Aidha alifahamisha kuwa waliofanya kitendo hicho wafahamu kuwa wamefanya jambo baya na kama wanahisi  kuwa Sheikh Soraya amefanya kosa  wajibu wao ni kumwita na kumuelekeza kama dini ya kiislamu inavyosisitiza.

Amesema bila shaka hizo ni chuki binafsi na sio masuala ya uislamu na si vizuri kumuhusisha mtu  na jambo lolote bila ya kufanya uchunguzi kwani unaweza kumfikiria mtu jambo ambalo  halimusu .

Alieleza  kuwa kujeruhiwa kwa Sheikh Soraga ni mbinu za makusudi zilizoandaliwa na watu kwani awali  aliwahi kufuatwa na maadui zake akitokea Mazizini  kuelekea Malindi lakini walipofika Hailesalases dereva wake alibaini kuna gari inawafuata na aliamua kubadili njia  na kupita Bustani ya Jamuhuri na maadui hawo wakatoweka.

Hata hivyo Naibu Mufti alisema dereva huyo hakuweza kuitambua gari ambayo ilikuwa ikiwafuata.  Sheikh Soraya ameathirika sehemu ya usoni, kifuani na tumboni na hali yake ina endelea vizuri na amepelekwa Dar es Salamu katika Hospitali ya rufaa ya Muhimbili kwa matibabu .
Posted by MROKI On Tuesday, November 06, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo