Nafasi Ya Matangazo

September 03, 2012

Waweza dhani watu hawa wapo katika foleni ya kupiga kura au kusubiri kujiandikisha kwaajili ya vitambulisho vya Utaifa..la hasha bali foleni hii ndefu ambayo huanzia majira ya alfajiri hadi usiku  wakati mwingine ni ya baadhi ya wakazi wa Ukonga jijini Dar es Salaam waliojipanga jana kupata huduma ya LUKU.

Tangu Septemba 1, 2012 Shirika la Ugavi la Umeme Tanzania (TANESCO) waliutangazia umma wa Watanania kuwa kutaanza zoezi la uboreshaji wa mfumo wa LUKU nchini. Kuanza kwa zoezi hili kumefanyika huku wananchi wakipata adha kubwa ya kukaa katika foleni kwa muda mrefu na wengine kukata tamaana kulala gizani katika nyumba zao.

Hali hii hasa ina lalamikiwa kutokana na Shirika hilo kuwa na vituo vichache vya kuuzia umeme jijini Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla. Hivyo shirika halina budi kuongeza pia vituo.
Posted by MROKI On Monday, September 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo