Nafasi Ya Matangazo

September 19, 2012

Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama barabarani leo wametembelea maeneo mbalimbali ambayo yamekuwa yakitokea ajali mara kwa mara katika barabara kuu ya Morogoro-Iringa-Mbeya na kupeana ushauri juu ya hatua za kuchukua katika kupunguza ajali hizo.

Pichani ni Kamanda wa Trafiki Mkoa wa Iringa, Mrakibu wa Polisi Pamphil Honono akiwaonesha wajumbe hao maeneo hayo wakati wamesimama katika kijiji cha Lugalo mkoani Iringa ambako ndio kuna kona ya mwisha ya Mlima kitonga. Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalkama Kitaifa yanafanyika mkoani Iringa na Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
Mmoja wa wajumbe hao akitoa ushauri kwa kikosi cha Usalama barabarani mkoani Iringa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Iringa, Salim 'Asas' Abri.
Kamanda wa Trafiki Mkoa wa Iringa, Mrakibu wa Polisi Pamphil Honono (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani mkoa wa Iringa, Salim ‘Asas’ Abri wakati wa ziara hiyo.
Lori la mizigo lililosheheni mbao likiteremka mlima Kitonga hii leo. Askari wa Usalama baarabarani wametakiwa kuongeza doria katika mlima huo kufuatia ajali za mara kwa mara zinazotokea kutoka na madereva kuendesha kwa fujo bila kuzingatia usalama barabarani.
Mteremko wa Mlima Kitonga
Basi la Taqwa likiwa limehariba katika mlima Kitonga leo.
Wajumbe wa Baraza wakimpa maelekezo OCD wa Kilolo juu ya kudhibiti ajali katika mlima Kitonga.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga akichukua picha katika mlima kitonga
Wajumbe wa Baraza la Wiki ya Nenda kwa Usalama wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha ziara yao ya kutembelea mliama Kitonga. Maadhimisho ya wiki ya Nenda  kwa Usalama kitaifa yanafanyika Mkoani Iringa  na
Posted by MROKI On Wednesday, September 19, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo