Nafasi Ya Matangazo

July 04, 2012

 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wameanza ziara ya siku mbili Washington DC, kuanzia tarehe 2 - 4 Julai 2012. Pichani, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwneye ubalozi wa Tanzania Washington DC.
 Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Lilly Munanka akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) kwenye ofisi za ubalozi
 Kaimu Balozi wa Tanzania Mhe. Lilly Munanka akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walioanza ziara ya siku mbili Washington DC 
Baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi wakipata picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo 

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.)akifuatilia taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania Moscow, kutoka kwa mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa aliyejumuika na msafara huo akitokea  Moscow.
Posted by MROKI On Wednesday, July 04, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo