Nafasi Ya Matangazo

July 31, 2012

Mchuuzi wa viatu katika mitaa ya jiji la Arusha, akipanga viatu vyake tayari kwa kusubiri wateja kandokando ya barabara jambo ambalo wakati mwingine huleta tabu kwa watembea kwa miguu kupita. Serikali kupitia Halmashauri hazina budi kutenga mazingira mazuri kwa wafanya biashara wadogo kama hawa ili waweze kufanya shughuli zao bila usumbufu.
 Mkazi wa Arusha akipita kando ya viatu vya mitumba vilivyopangwa kando ya barabara. Wauzaji wengi wa viatu na nguo katika miji mingi wamekuwa wakipanga vitu vyao kando ya barabara.
Mkazi wa Arusha akipaka nakshi kandambili iliyotengenezwa kwa matairi chakavu ya magari. Aina hiyo ya Kandambili ambayo ilikuwa ikitumiwa zaidi nchini miaka ya nyuma imeanza kushika kasi tena kwa kupendwa na watu wengi kuvaliwa hasa mijini kutokana na uimara wake tofauti na kanda mbili zinunuliwazo madukani. Utengenezaji na uuzaji wa viatu hivi umeleta ajira na kukuza kipato kwa vijana wengi.
Posted by MROKI On Tuesday, July 31, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo