Nafasi Ya Matangazo

June 04, 2012

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao leo Juni 4, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha. Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kesho ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza  na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao leo Juni 4, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha.Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kesho ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao.

********
Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt Jakaya Mrisho kikwete,  mchana huu Juni 4, 2012 amekutananaWabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashari kijijiniArusha.

Mhe.Rais, ambaye aliwakaribishaWabunge hao kwa chakula cha mchana katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge, aliwapongeza kwa kuchaguliwa kwao kuiwakilisha Tanzania katika Bunge hilo la Jumuiya, na kuwataka wasimamie na kutetea maslahi ya nchi wakiwa huko.

Pia Rais amewataka Wabunge hao kuwa karibu na Serikali katika kushauriana namna ya kukabiliana na changamoto zitazojitokeza katika kazi zao, na kuwakumbusha kwamba majukumu ya Bunge hilo la Jumuiya ni kusimamia makubaliano  (treaty) yaliyoyoorodheshwa katika kuundwa kwake na kuendeshwa.

Alisema: “Msome vyema na kuyaelewa makubaliano (treaty) hayo yote na vipengele vyake na msaidie kuiendeleza Jumuiya ambayo wanachama wote watanufaikanayo, na siyo upande mmoja.

“Tumewapeleka pale kwaajiliyamaslahiya Tanzania hivyomjuekunakazinyingikweli,   hasa katika kujadili yale yote yaliyokubaliwa katika makubaliano ya jumuiya” alisema.

Mhe.Rais alikutana na Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki isipokuwa mmoja, Bi. Nderkindo Perpetua Kessy ambaye hakufika kwasababu iliyoelezwa kuwa ni mgonjwa. Waliofika ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabungewa Tanzania kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose SaddrudinBhanji.

WenginewaliofikaniMhe. AnjelaCharlessKizigha, Mh. Maryam UssiYahya, DktTwahaIssaTaslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard MusomiMurunyanaMhe. Charles MakongoroNyerere.

Wabunge ha owanatarajiwa kuungana na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi keshoJuni 5, 2012 katika kikao chao rasmi cha kwanza ambapo watamchagua Spika na kisha kula viapo kabla ya kuanza majukumu yao.

Imetolewana:

KurugenziyaMawasilianoya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
04 Mei, 2012.
Posted by MROKI On Monday, June 04, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo