Nafasi Ya Matangazo

June 04, 2012

Historia inaonyesha kwamba wanamuziki wengi hupitia vikwazo vingi mpaka kufikia mafanikio. Ni hali halisi ambayo bila shaka inaeleweka ukizingatia utitiri wa vijana wenye vipaji vya kuimba na hata kutunga au kuandika nyimbo. Wapo wengi.Katika sanaa ya muziki kuna kukataliwa, kuna kuambiwa huwezi, hujui kitu na huwezi kufika mbali.

Pamoja na ukweli huo, kuamua kuendelea au kukubaliana na “maoni” ya wadau na kuachana na muziki, kunategemea mambo kadhaa ikiwemo imani binafsi kama unaweza au huwezi. Ukiambiwa huwezi na wewe ukakubaliana na hoja hiyo,bila shaka utakuwa umefikia mwisho wa ndoto.Unaamka.

Lameck Ditto ni miongoni mwa wanamuziki ambao wamepitia vikwazo vingi mpaka kufikia hapo alipo hivi leo. Bila shaka tunakubaliana kwamba Ditto  ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye vipaji, nidhamu na juhudi za hali ya juu katika sanaa ya muziki.

Kufikia hapo alipo, alipitia mengi. Alistahimili mengi. Aliwahi kuambiwa hawezi. Aliwahi kutembea kwa mguu masafa marefu ili kwenda studio kwa sababu mfukoni hakuwa na nauli hata ya daladala. Kukaja masuala binafsi ya kufiwa na Mama yake mzazi akiwa bado kijana mdogo tu. Kwa muda mrefu hakumjua baba yake. Akaishi kwa kubahatisha kama vile mtoto wa mtaani. Pamoja na yote hayo,akaendelea kuamini kwamba anaweza na sanaa ndio itakayomtoa. Kama alivyoimba katika wimbo wake “Tushukuru Kwa Yote”, Ditto akaendelea kushukuru na sasa anaanza kuonja mafanikio ya uvumilivu;

Nini kinamfanya kamwe asikate tamaa? Baada ya kufikia mafanikio ambayo anayo hivi sasa,ana mipango gani? Ilikuwaje akaamua kwamba sanaa ya muziki ndio uwanja wake wa kujidai? Fuatana nami katika mahojiano yangu na Lameck Ditto, akielezea kule alikotoka,alipo na anapotaraji kufika na mengine mengi;

BC: Hello Ditto,karibu sana ndani ya BC.Tunafurahi kuwa nawe hivi leo.Labda kwa haraka na kwa faida ya msomaji ambaye hakufahamu, unajielezeaje? Ditto ni nani.Ni mtu wa aina gani?


LD: Asante sana Jeff.Nami nafurahi sana kuwa nawe ndani ya BC. By the way unafanya kazi nzuri sana.

Kwa kifupi tu Ditto ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo. Ni kijana ambaye anajitahidi kujituma katika shughuli zake yeye binafsi na pia kutoa msaada katika shughuli za wenzake kila anapohitajika na kila inapowezekana. Ni kijana mwenye imani katika kufanikiwa bila kujali chochote kinachohusiana na ugumu wa kufanikisha jambo.Ni mpole,mcheshi,msikivu na anayependa kujiendeleza.Huyo ndio Ditto.

BC: Mara nyingi wasanii huanza kupenda aina fulani ya muziki kutokana na waimbaji au wanamuziki walioanza kuwasikiliza tangu wakiwa watoto.Kwa upande wako unakumbuka ulipenda kusikiliza miziki ya kina nani au bendi gani? Unadhani miziki hiyo ilichangia katika uamuzi wako wa kufanya aina ya muziki unaofanya hivi leo?

LD: Kama kijana mwingine yeyote, nilipenda kusikiliza muziki. Na hata nisingependa wakati nazaliwa televisheni zilikuwa bado sio maarufu kwa hiyo nyumbani ukiingia utakachosikia ni redio na mara nyingi redio na muziki na mtu na nduguye. Kwa hiyo niliwasikiliza wanamuziki wengi.

Lakini ambao naweza kusema walinivutia zaidi ni wanamuziki kama vile  Hayati Marijani Rajabu kwa upande wa wanamuziki wa kizazi cha awali na watu kama Banana Zorro,Lady jaydee Na Prof J kwa upande wa wale wa kizazi kipya.

Read more: LAMECK DITTO: ALIPOTOKA,ALIPO NA ANAPOOTA KUFIKA(INTERVIEW) - BongoCelebrity .
Posted by MROKI On Monday, June 04, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo