Nafasi Ya Matangazo

May 15, 2012

REDD’S MISS KURASINI 2012

Mashindano ya REDD’S MISS TANZANIA 2012 yanaendelea kushika kasi kwa ngazi za vitongoji hapa jijini Dar es salaam, Baada ya kufanyika kwa mashindano katika kituo cha UKONGA, CHUO CHA USTAWI WA JAMII na CHUO CHA FEDHA (IFM) sasa ni zamu ya REDD’S MISS KURASINI 2012.

Katika mashindano ya mwaka huu kituo hiki cha Kurasini kitafanya shindano lake siku ya Ijumaa ya tarehe 25 / 5 / 2012 katika Ukumbi wa EQUATOR GRILL uliopo mtoni saba saba.

Jumla ya Warembo kumi na sita mpaka sasa wamejitokeza katika kuwania taji la REDD’S MISS KURASINI 2012 ambalo linashikiliwa na MWAJABU JUMA  ambaye pia ni mshindi wa shindano la TOP MODEL 2011 katika fainali za Miss Tanzania 2011, pia ni miongoni mwa warembo waliofika katika fainali ya mashindano ya urembo ya MISS TANZANIA 2011.

mazoezi ya warembo wa Miss Kurasini 2012 yanaendelea katika ukumbi huo wa Equator Grill chini ya walimu wao Top Model MWAJABU JUMA na ROSE HERBERT kwa upande wa SHOO,

Orodha ya majina ya warembo na umri wao ni kama ifuatavyo:-

1.   TULEKENE SETH (20)               2. ANGLE GASPER (19)
3.   CHRISTINA MOSES (22)           4. ZUHURA SADIKI (21)
5.   FLAVIANA MAEDA (22)            6. MWANAISHA ZUBERI (21)
7.FARIDA MROPE (23)                     8. IRENE SOSTHENES (20)
9. EDINA MAGIGE (22)                   10. SIA KIMAMBO (19)
11. NZELANI JUMA (22)                  12. LILIAN JOSEPH (20)
13. ANNA ZAKARIA (21)                  14. ASHA MUSA (21)
15. LINDA DEUS                                 16.BETTY PETER (22)


ZUWENA MUSTAPHA
MKURUGENZI.
Posted by MROKI On Tuesday, May 15, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo