Nafasi Ya Matangazo

April 05, 2012

MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.

Taarifa kutoka jijini Arusha zinasema uamuzi huo umefikiwa leo asubuhi Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo. 


Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).


Lema katika Uchaguzi huo alikuwa akichuana vikali na Mgombea wa CCM, Dk. Batilda Salha Buruiani ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya.

Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cham hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.

Pia habari za ndani ya Chama cha Chadema zinasema kuwa tayari Chama hicho kilisha soma alama za nyakati mapema katika kesi hiyo miezi kadhaa nyuma na kujipanga endapo mbunge huyo atavuliwa wadhifa wake nani kimsimamishe kutetea kiti hicho.

Habari hizo zinadai kuwa Chadema kimepanga kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chama hicho na Mgombea Urais wa 2010, Dk. Wilbroad Silaa kutetea kiti hicho.Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa  wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.

Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5 kujitetea.

Father Kidevu Blog itaendelea kukupa habari zaidi za Hukumu hiyo. 
Posted by MROKI On Thursday, April 05, 2012 7 comments

7 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo