Nafasi Ya Matangazo

February 09, 2012

Afisa Uhusiano wa TACAIDS Grory Mzirai akitoa mada katika semina ya kuwajengea uwezo waandaji wa vipindi vya Redio na Watangazaji kwa Kanda ya Mashariki inayofanyika kwa siku mbili kwenye hoteli ya Kibaha Confernce Center Maili moja Mjini Kibaha.

Waratibu wa Ukimwi katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Lindi na Mtwara wapo kwa ajili ya kuwaelezea masuala mbalimbali washiriki wa semina hiyo,  kuhusu maambukizi ya ukimwi na kupambana na janga zima la Ukimwi linalotishia jamii na nyanja mbalimbali za  kiuchumi nchini Tanzania kutokana na kudhoofisha nguvu kazi ya Rasirilimali watu.

Semina hiyo imeandaliwa na Taasisi ya kuzuia ukimwi TACAIDS ikishirikiana na kampuni ya Masoko Agency ya jijini Dar es salaam  na tayari imeshafanyika katika kanda Kaskazini Arusha, Kanda ya Ziwa Mwanza, Kanda ya Kati Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya na sasa ni Kanda ya Mashariki Mjini Kibaha
Lugano Henry Meneja Mawasiliano na Mafunzo wa kampuni ya Masoko Agency akizungumza katika semina hiyo inayofanyika kwa siku mbili katika hoteli ya Kibaha Conference Center mjini Kibaha.
Bw. Simon Keraryo Afisa Uhamasishaji (TACAIDS) naye alizungumzi mambo kadhaa katika semina hiyo kama anavyoonekana katika picha.
Mmoja wa watoa Mada ambaye pia ni mtangazaji wa ITV Bw. Godwin Gondwe (kushoto)  akiteta jambo na Meneja Mawasiliano na Mafunzo Lugano Henry.
Regina Mwalekwa Mtangazaji kutoka Redio Clouds kulia kulia akiwa pamoja na Jacqueline Chengula mtangazaji mwenzake kutoka Clouds wakiandika mambo muhimu yaliyokuwa yakijitokeza wakati watoa mada wakiendelea na mada hizo katika semina ya waandaaji wa vipindi vya redio na watangazaji mjini Kibaha.
Kutoka kulia ni Hafidh Ameir mratibu wa TACAIDS mkoa wa Pwani, Joel Mnanga Mratibu wa TACAIDS Mtwara na Afisa Uhusiano wa TACAIDS Grory Mziray wakibadilishana mawazo katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini masuala mbalimbali katika semina hiyo.
Posted by MROKI On Thursday, February 09, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo