Nafasi Ya Matangazo

January 18, 2012

Rais Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Regia Mtema aliyekuwa mbunge wa CHADEMA viti maalum kutoka mkoani Morogoro, Regia Mtema amezikwa Ifakara mkoani humo leo huku mazishi yake yakihudhuriwa na viongozi wa Serikali na Bunge pamoja na wanasiasa na ndugu jamaa na marafiki hii leo., Marehemu Regia alifariki kwa ajali ya gari iliyotokea Ruvu mkoani Pwani siku ya jumapili
Rais Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akiwa na viongozi wa Bunge, Serikali na Vyama vya siasa wakati alipoongoza wananchi katika mazishi ya Marehemu Regia Mtema huko Ifakara Mkoani Morogoro kutoka .kulia ni Hawa Ghasia Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Job Ndugai Naibu Spika wa Bunge, Spika wa bunge Anne Makinda na kutoka kushoto ni Zitto Kabwe Mbunge wa Chadema Kigoma Kaskazini, Freeman Mbowe mwenyekiti wa CHADEMA na Joel Bendera Mkuu wa mkoa wa Morogoro.
Wakazi mbalimbali wa mji wa Ifakara waliohudhuria mazishi ya Marehemu Regia .
Rais Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Regia Mtema aliyezikwa leo Ifakara mkoani Morogoro.
Rais Kikwete akienda kuweka shada la maua juu ya kaburi la Marehemu Regia Mtema.
Posted by MROKI On Wednesday, January 18, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo