Nafasi Ya Matangazo

August 25, 2011

Mkazi wa Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, Ally Kidunda, akizungumza katika mkutano wa hadhara uliokuwa uzikutanishe pande mbili za wakulima wa kijiji hicho na mzungu anayemiliki kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayodai kununua shamba katika kityongoji cha Kinyenze na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia yakwenda mtaa wa Mwanga.
Mkazi wa Kinyenze Hadija Mwinyipembe akizungumza katika mkutano huo. Hadija alilalamikia kitendo cha kufungwa kwa njia hiyo na kuamriwa kuhamisha makaburi ya wazazi wao yaliyopo kijijini hapo.
Mmsimamizi wa mzungu anaesimamia shamba hilo aliyetambulika kwa jina la Mbaraka akiwa na Mwenyekiti wa Kijiji Anthoni Karoli (aliyeketi) hata hivyo Mbaraka alitimuliwa na wananchi katika enbeo la mkutano.
Mbaraka akiondoka katika gari
Baadhi ya Wananchi wa Kitogoji cha  Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, wakipita  pembezoni mwa uzio wa senyeng’e iliowekwa na kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa  Raia wa kigeni aliyeuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia yakwenda mtaa wa Mwanga kama walivyokutwa juzi Kijijiji hapo.
Njia kuu itumikayo na magari kwenda katika Mtaa wa Mwanga ulio na kaya zaidi ya mia moja ambayo nayo imefungw na mzungu huyo. Wananchi wameitaka serikali ya Wilaya na Mkoa kuingilia kati mgogoro huuo haraka kabla wao hawajatumia sheria mkononi kuvunja uzio huo.
Bibi Mawazia Kibwana , mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, akitoa malalamiko kuhusu kubomolewa choo chake na kuwekwa kwa uzio wa seng’enge na kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa  Raia wa kigeni aliyeuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia yakwenda mtaa wa Mwanga kama walivyokutwa juzi Kijijiji hapo.
moja ya nyumba ambazo uzio umepita na kuziba vyoo vyao.
wananchi wakiangalia eneo la shule ya Msingi Kinyenze ambayo nayo imezungushiwa uzio.
Wananchi wakipita jirani na Jumba ambalo awali watoto walikuwa wakilitumia kama darasa la chekechea ambalo sasa linamilikiwa na mzungu huyo.
Posted by MROKI On Thursday, August 25, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo