Nafasi Ya Matangazo

March 16, 2011

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Shamsi Vuai Nahodha (katikati) akiwa pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Saidi Ali Mwema (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, Matanga Mbushi wakitoa salam wakati kikundi cha bendera akilipokua kinapita mbele yao. Mhe. Waziri alikua mgeni rasmi katika mahafali ya kuhitimu kwa askari polisi jana katika Chuo cha Polisi Moshi. Jumla ya askari 2847 wamehitimu mafunzo ya awali wakiwemo askari wa uhamiaji 115.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Shamsi Vuai Nahodha akikagua gwaride la askari Polisi na Uhamiaji waliomaliza mafunzo ya awali katika Chuo cha Polisi Moshi.
 Askari Polisi wakiwa katika onyesho la karate jana mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro wakati wa mahafali ya kumaliza mafunzo ya awali ya askari Polisi na Uhamiaji.
 Askari Polisi mlengaji  akiwa katika onyesho la vikwazo ambapo askari huyu ni mmoja kati ya askari polisi 2732 waliohitimu mafunzo ya awali jana katika Chuo cha Polisi Moshi ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani alikua mgeni rasmi.
 Askari wa Kikosi cha farasi wakipita mbele ya mgeni rasmi Mh. Shamsi Vuai Nahodha wakati wa mahafali ya kumaliza mafunzo ya askari Polisi na Uhamiaji katika Chuo cha Polisi Moshi.
 Askari wa kikosi cha kupambana na majanga wakiwa katika harakati za kuzima moto wakati wa onyesho la kupambana na majanga jana katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi.
Posted by MROKI On Wednesday, March 16, 2011 2 comments

2 comments:

  1. Mmmhhh!

    Huo moto mbona walishindwa kuuzima ule wa Mabomu ya Gongo La Mboto kule!?

    ReplyDelete
  2. Mh,kaka hata mi nna daut meeen!Au hao jamaa masharobaro men..Eti kaka wengine wataenda mosh(CCP) lini baada ya hawa wa march 2011

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo