Nafasi Ya Matangazo

December 22, 2008

Aliyepandisha Bendera na Mwenge wa Uhuru kwa mara ya kwanza katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro katika kuazimisha Uhuru wa Tanganyika Brigedia Alexanda Nyirenda (72) amefariki dunia.
Nyirenda ambaye aliopandisha mwenge huo usiku wa Desemba 9,1961 alifariki mwishoni mwa wiki jana alipokuwa anauguzwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na anatarajiwa kuzikwa Jumatano wiki Hii katika makaburi ya Kinondoni. Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es Salaam. Nyirenda amefariki siku chache baada ya tanzania kuazimisha mika 47 ya Uhuru. Azaliwa Februari 2 1936 huko Kaonga Malawi. Alisoma Shule ya Msingi Mchikichini na baadae Sekondari ya Malangalali na kumalizia Tabora Boyz.
Marehemu ameacha mjane, watoto watano na wajukuu 10.
Brigedia Alexanda Nyirenda(kulia) akisalimiana na Naibu Mhariri wa TSN Mkubwa Ali alipokuwa katika mahojiano maalum na gazeti hili tarehe 30/11/2006 katika ofisi za gazeti la HabariLeo. Father Kidevu nilipiga picha hizi na nyinginezo.
Mungu ailaze roho ya Shujaa huyu mahali pema Amina.

Posted by MROKI On Monday, December 22, 2008 4 comments

4 comments:

  1. KAKA NAKUSHUKURU SANA KWA KUWEKA PICHA ZA MZEE NYIRENDA ZA SASA HAO WENGINE WAMEMWEKA PICHA ZA ZAMANI SANA .
    NAPENDA KUTOA SALAMU ZANGU ZA RAMBIRAMBI KWA JIRANI YETTU HUYU WA ZAMANI . NYIRENDA ALIISHI MUDA MREFU SANA ZAMBIA NA ALIRUDI TANZANIA MWAKA KAMA SIKOSEI 1994.
    NI MTOTO WA DADA WA RAISI KAUNDA WA ZAMBIA NA HUYU MZEE NDIGU ZAKE WOTE NI WALE WANYASSA AMBAO WALITINGISHA NCHI ENZI HIZO DR MTAWALI KAMA ULIMSIKIA . PROFESSOR SHABA NA KAMANGAS .POLENI SANA

    ReplyDelete
  2. NAPENDA KUMPA POLE ALEX GONDWE AMBAE YUPO INDIA KWA MSIBA HUU MAANA MWARA MYINGI SANA NILIKUWA NAMWONA KWAO

    ReplyDelete
  3. MBONA PICHA ZA NYIRENDA HUJAWEKA WEWE KIDEVU MBONA HAUPO COMPETATIVE NA BLOGU ZINGINE

    ReplyDelete
  4. HUYU NYIRENDA ALIKUWA ANATAKA KUPINDUA NCHI

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo